💻

Mfuko wa Maendeleo wa Zcash

Zcash ni itifaki ya blockchain ya kipekee kwa sababu inajifadhili yenyewe. Hii inamaanisha kuwa timu zinazofanya kazi kwenye Zcash hazihitaji kupata pesa kutoka kwa wawekezaji wa nje, na wanaweza kuendelea kuwa na lengo la kuchochea kukubalika wakati pia wakizingatia maadili na malengo mapana ya Zcash.

Tuzo za Vizuizi/Block Rewards

Katika blockchain, kuna kitu kinachoitwa vizuizi,ambavyo huzalishwa ili kurekodi shughuli ambazo bado hazijathibitishwa kwenye mtandao. Mara tu shughuli zinapothibitishwa, kizuizi hufungwa.

Wazalishaji wa vizuizi (inayojulikana pia kama wachimba madini) wamepewa jukumu la kuthibitisha shughuli kwenye mtandao na kuzalisha vizuizi vipya. Wanapozalisha vizuizi hivyo, wazalishaji wa vizuizi hupokea tuzo ya kizuizi. Katika Zcash, kwa kiasi kikubwa kila sekunde 75 kuna kizui kipya kinachozalishwa, na tuzo ya kizuizi ya 3.125 ZEC huingia katika mzunguko. Tuzo za vizuizi kwenye Zcash zitasababisha sarafu mpya kuzalishwa hadi Zcash ifikie ugavi wake wa juu wa milioni 21. Baada ya kufikia ugavi wa juu, tuzo za vizuizi zitalipwa kwa njia ya ada za shughuli.

Mfumo wa ufadhili wa kipekee wa Zcash

Katika Bitcoin na sarafu nyingine za sarafu, tuzo zote za vizuizi huenda kwa wazalishaji wa vizuizi. Zcash ni tofauti kwa sababu 20% ya tuzo ya kizuizi hutolewa kwenye mfuko wa maendeleo ya Zcash. Mfuko huu hufadhili timu zinazofanya kazi kwenye itifaki ya Zcash.

Kwa sasa, Zcash Community Grants hupokea 8% ya tuzo za vizuizi, Electric Coin Co. 7%, na Zcash Foundation hupokea 5%. Hii inafanya jumla ya 40%, 35%, na 25% ya mfuko wa maendeleo mtawaliwa.

image

Dev Fund Recipients

Mwaka 2020, jamii ya Zcash ilipiga kura juu ya mfuko wa maendeleo na timu zilizoungwa mkono na mfuko huo. Mwaka 2024, jamii itapiga kura tena ili kuamua ni nani atapata ufadhili kutoka kwenye mfuko wa maendeleo.

Rasilimali