Taasisi ya Zcash/ Zcash Foundation

Taasisi ya Zcash/ Zcash Foundation

Tamko la Malengo

Lengo la Taasisi ya Zcash ni kuwa shirika la hisani ya umma lenye kujitolea katika kujenga miundombinu ya malipo na faragha kwenye mtandao kwa faida ya umma, kwa kuhudumia hasa watumiaji wa itifaki na blockchain ya Zcash.

Watu na Timu

Taasisi ya Zcash ina karibu wafanyakazi 15 ambao wametawanyika ulimwenguni. Wao hufanya kazi katika maeneo mbalimbali kama maendeleo ya itifaki, usalama wa itifaki, maendeleo ya biashara na usimamizi wa matukio ya jamii ya Zcash.

Timu ya ZF inajumuisha bodi ya wakurugenzi, timu ya uhandisi, na timu ya uendeshaji.Habari zaidi hapa.

Ruzuku za Taasisi ya Zcash zinasaidia mfumo wa ikolojia kwa kutoa njia ya kufadhili miradi ambayo inachangia katika ikolojia ya faragha, kama vile Zebra (utekelezaji huru wa node kwa Zcash) & FROST.

Taasisi pia inaandaa Zcon, mkutano wa kila mwaka unaofanyika ana kwa ana na unalenga ikolojia ya Zcash. Pia, inasaidia jitihada za jamii kama vile Zcash Foundation A/V Club.

Muundo wa Shirika

Taasisi ya Zcash ni shirika lisilo la faida la aina ya 501(c)(3). Mbali na timu yao, wanayo pia bodi ya wakurugenzi.

Ufadhili

aasisi ya Zcash hupokea asilimia 5% ya Mfuko wa Maendeleo wa Zcash. Matumizi ya fedha zao yanaweza kuonekana katika Ripoti za uwazi/transparency reports ambazo hutoa kila robo mwaka.

Rasilimali